
SportPesa Tanzania yasaini upya udhamini wa Yanga: Mashabiki waupokea kwa shangwe ushirikiano huu mkubwa
Harakati kubwa kwenye anga la michezo nchini Tanzania — ni huu si uvumi tu, bali ni uthibitisho wa dhamira ya kweli. Kupitia SportPesa Tanzania, kampuni inayoongoza michezo ya kubashiri kidijitali barani Afrika, imeimarisha nafasi yake si tu kwenye uwanja wa burudani, bali pia kwenye mustakabali wa soka la Tanzania.
Hii ni zaidi ya mkataba; ni makubaliano ya kihistoria yanayoendeleza ushirikiano wa miaka mingi kati ya SportPesa Tanzania na Young Africans SC (Yanga). Ni tangazo lililopokelewa kwa shangwe kubwa na mashabiki kote nchini — shangwe inayoshuhudia urithi, uthabiti na upeo mpya wa maendeleo ya michezo.
Akizungumzia makubaliano hayo mapya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya SportPesa Tanzania, Abbas Tarimba alisema: “Dhamira ya Sportpesa ilikuwa na ndoto kuingia kwenye mpira. Tuliwahi kudhamini Arsenal, Hull City, Everton na Ligi Kuu Kenya klabu kadhaa.”
Akaendelea na kusema, “Tulipotazama Tanzania tukabaini Yanga ni Klabu sahihi kutimiza nayo ndoto zetu. Yanga ina mashabiki wengi. Tuliwaamini sana viongozi wa Yanga kwamba tungeubadilisha mpira wa Tanzania. Baada ya sisi kuingia Yanga, tuliwapa nguvu ya kiuchumi.”
Nguvu ya ushirikiano
Udhamini wa Sportesa kwa timu ya Yanga imekuwa injini kuu ya mafanikio ya klabu hii kongwe barani Afrika Mashariki. Kupitia udhamini huu, Yanga FC imejiimarisha kama klabu yenye heshima kubwa, sio tu ndani ya Tanzania, bali pia kwenye mashindano ya kimataifa.
Mashabiki wameona matunda ya moja kwa moja ya ushirikiano huu: uwekezaji katika vifaa vya kisasa, programu za maendeleo ya vijana, na miundombinu inayokuza vipaji vya nyota wa kesho. Hii si hadithi ya maneno matupu — ni ushahidi wa jinsi SportPesa inavyoendelea kubadili taswira ya michezo nchini.
Sauti za viongozi wa Yanga
Kwa niaba ya uongozi wa Taasisi ya Yanga SC, Rais Hersi Said naye alinena: “Kabla ujio wa Sportpesa Yanga ilikwama. Licha ya ukubwa na ukongwe wake, Yanga ilishindwa kupata wachezaji wazuri, Yanga ilishindwa hata kusafiri bila changamoto. Lakini leo hii Yanga inagombea wachezaji wazuri na klabu kubwa Afrika.”
“Haikuwa kazi rahisi, zilikuwepo kampuni nyingi, lakini ofa ya SportPesa ndiyo ilikuwa bora zaidi. Kwanini SportPesa? Ni kwa sababu hii ni Kampuni ya Kubeti ambayo haina longolongo, pia wanafanya mambo kwa kuzingatia taaluma. Lakini kubwa aidi tumepata mafanikio makubwa Pamoja,” Alisema Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga.
Mafanikio yanayoonekana
Kupitia udhamini wa kampuni bora ya kubeti kwa timu ya Yanga, mashabiki wameona:
- Uimarishaji wa miundombinu ya klabu na vifaa bora.
- Kuwepo kwa programu za kukuza vipaji vya vijana.
- Uboreshaji wa hadhi ya Yanga kwenye mashindano ya kimataifa.
- Fursa za kijamii kupitia Shabiki ambazo zimegusa maisha ya mamia ya Watanzania.
Enzi mpya kwa Yanga na Tanzania
Kupitia kuendelezwa kwa udhamini wa Yanga FC, Tanzania inaingia katika enzi mpya ya michezo yenye matarajio makubwa. Ushirikiano huu ni zaidi ya mkataba wa kifedha — ni agano la matumaini, maendeleo na mshikamano kati ya klabu kongwe ya Yanga, mashabiki wake, na kizazi kijacho cha michezo.
Zaidi ya soka: Shabiki
Ushirikiano huu unapanuka zaidi ya viwanja vya michezo. Kupitia mpango wa Shabiki, SportPesa Tanzania inaendelea kuwekeza kwenye jamii. Shabiki inalenga kusaidia timu za mitaani, miradi ya kijamii, na vipaji vinavyoibukia ili kuhakikisha kwamba michezo inabaki kuwa chombo cha maendeleo ya kijamii.
Iwe ni timu ndogo kijijini, kundi la vijana wabunifu, au mradi wa kijamii wenye athari kubwa — SportPesa Shabiki iko mstari wa mbele kuinua ndoto na kuzigeuza kuwa halisi. Kula gemu kwa ujanja, usiwaze bando ukiwa na laini za Voda, Yas, ama Tigo. Kupitia Selcom, unaingiza mshiko easy.